Pages

Ads 468x60px

.

About

.

Wednesday, August 8, 2012

WB yaipa Ilala Sh41Bilioni kuboresha miundombinu

BENKI ya Dunia (WB) imetoa mkopo wa Sh41 bilioni kwa ujenzi  wa miundombinu Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.

Fedha hizo ni sehemu ya Sh150 bilioni ambazo ziliombwa na halmashauri nne za Dar es Salaam kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la madiwani,  Meya wa Ilala, Jerry Silaa alisema Serikali iliomba mkopo WB kutekeleza miradi mbalimbali ya kuboresha miundombinu ya Da es Salaam.

Slaa alisema miundombinu hiyo ni barabara, mifereji ya maji, uzoaji taka, urasimishaji makazi, uboreshaji mapato ya halmashauri, ujenzi wa miundombinu kwenye makazi yasiyopangwa na utawala bora.

“Uboreshaji miundombinu ya barabara na mifereji ya maji ya mvua, zimetengewa Sh21 bilioni, ukusanyaji na usafirishaji taka ngumu umetengewa Sh5.3 bilioni, uboreshaji miundombinu kwenye makazi yasiyopangwa Sh 8.4 bilioni,” alisema Slaa na kuongeza:

“Urasimishaji na kutenga maeneo ya huduma kwenye makazi yasiyo rasmi imetengwa Sh1.6 bilioni.” 
Pia, alisema mradi huo ni wa awamu ya kwanza ambayo itahusisha kata za Kiwalani, Gongolamboto  na Ukonga na kwamba, wakimaliza wataingia awamu ya pili.

“Uboreshaji huo utakuwa Kata ya Kiwalani mitaa ya Minazi mirefu, Yombo, Kiwalani na Kigilagila; Kata ya Gongolamboto itahusu mitaa ya Gongolamboto, Ulongoni, Guluka Kwalala na Mongolandege na Kata ya  Ukonga mitaa ya Makazi, Mazizini na Mwembe madafu,” alisema.

Naye Diwani wa Kata ya Kivule, Nyasika Getema alisema kwenye kata yake ametengewa Sh6.29 milioni  kwa ujenzi wa barabara ya Mombasa-Moshi bar.


Saturday, July 28, 2012

RAMBO AMZIKA MWANAE 


STAA, Sylvester Stallone Rambo, amemzika mtoto wake wa kwanza, Sage Stallone, ambaye alifariki baada ya kumeza madawa mengi. 

Sage ambaye amewahi kuigiza na baba wake katika filamu ya Rocky V, alifariki dunia mapema mwezi huu ikiwa ni siku chache kabla ya kufunga ndoa. 
Chanzo cha kifo chake hakijathibitishwa na daktari, isipokuwa maiti yake ilikutwa pembeni ya chupa tupu za vidonge zipatazo hamsini. Sage amefariki akiwa na umri wa miaka 36. 
Kama alivyo baba yake, naye alikuwa mwigizaji, mwongozaji na mtayarishaji wa filamu.


CHAMELEONE ATINGA UBALOZINI



Mwanamuziki wa Nchini Uganda,Jose Chameleone (ambaye hivi karibuni alikuwepo hapa nchini kwa shoo yake moja) leo amefanya maandamano mpaka Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda akiambatana na wapenzi wa muziki wake,kwa lengo la kutaka kurudishiwa Passport yake inayodaiwa kuwa inashikiliwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers,Erick Shigongo.


Hapa akizungumza na askari wa Ubalozini hapo.Inasemekana kuwa Shigongo aliamua kuchukua uamuzi huo wa kuchukua passport ya Jose Chameleone kwa kuwa Meneja wake alimtapeli kiasi cha dola 3500 kipindi cha nyuma hivyo ameamua kuzuia pasport yake mpaka atakapomleta Meneja wake huyo. Mwanamuziki Jose Chameleone akipiga gitaa lake na kuimba huku wapenzi wa muziki wake wakiwa wamemzunguka kushinikiza Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda kufanya taratibu za kuwezesha kupatikana kwa hati yake ya kusafiria (passport) inayoshikiriwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers,Erick Shigongo.






Tuesday, July 3, 2012


NHC KUUZA NYUMBA KWA BEI NAFUU


SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) lina mpango wa kujenga nyumba 15,000 hadi ifikapo mwaka 2015 na kuziuza kwa bei nafuu kwa wananchi wenye kipato cha chini.

Mkurungenzi Mkuu wa shirika hilo Nehemiah Mchechu alisema Jijini Dar es Salaam jana kuwa nyumba hizo zitaanza kuuzwa kati ya Sh25milioni hadi Sh40 milioni  kwa lengo la kumsaidia mwananchi wa kipato cha chini.

Baada ya kusaini mkopo wa Sh165 bilioni kutoka kwenye Taasisi tisa za kifedha,Mchechu alisema fedha hizi zitawasaidia katika mradi wa ujenzi wa nyumba na ununuzi wa ardhi ya akiba katika mikoa mbalimbali nchini.

“Nyumba tulizojenga zaidi ya 1,500 kwa mwaka huu  zimewalenga wananchi wa kipato cha chini yule ambaye atashindwa kununua nyumba ya Sh70,000 ataweza kununua nyumba za bei nafuu ambazo zitauzwa Sh25 hadi 40 milioni”alisema na kuongeza;

“Mradi huu wa ujenzi umeanza kutekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma ,Arusha na Dodoma huku miradi mingine ipo njiani kutekelezwa” alisema Mchechu

Pia alisema kati ya fedha hizo zilizotolewa  Sh23 bilioni zitapelekwa  kwenye ujenzi wa nyumba za bei nafuu ambazo nyumba hizo zitawalenga wananchi wa kipato cha chini.

Kwa upande wake  Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka alisema wananchi wametakiwa kununua nyumba badala ya kununua viwanja ili kuepuka gharama zisizokuwa na  msingi.

Waziri huyo alisema wananchi wataweza kukopa nyumba hizo ambazo mikopo yake italipwa kwa riba ya chini ili waweze kunufaika na mradi huo.

“Wananchi wanunue nyumba badala ya  kununua viwanja, hii  itamrahisishia kupunguza gharama ya kununua kiwanja na kujenga ambayo kiwango chake ni kikubwa”alisema Profesa Tibaijuka.
 Profesa Tibaijuka alisema kati ya nyumba hizo zinazojengwa asilimia 25 zitabaki kwa ajili ya watu ambao watahitaji kupanga.


Monday, July 2, 2012

UVUMI KUHUSU JUSTINE BEIBER


Kumenea kwa uvumi mbalimbali kuhusu mwimbaji huyu na amefikiria kuimba wimbo utakao shika mawazo ya jamii
Justine Beiber hivi karibuni anakabiliwa na shtaka kutoka kwa msichana kuwa yeye ni baba wa mtoto wake, Ilikuwa aibu kwa na vigumu kukubali kwa nyota huyu ambaye anakuwa. Sasa ameamua kutafuta njia mbadala itakayo weza jibu maswali yake kwa kuimba wimbo utakao ongelea matukio yalio muhusu Justine Beiber na atatoa ufafanuzi juu ya yote kwa njia ya mistari ya wimbo wake!

Justin Bieber amepokea umaarufu mkubwa kutoka kwa mashabiki ndani ya kipindi kifupi sana, sasa ana kwa ana atajitahidi kujisafisha kwenye skendo mbalimbali zilizo muhusu yeye.


MADEREVA WALIOKAMATWA ZAMBIA


CHAMA cha Madereva wa Malori (Chamamata) kimeiomba Serikali kufanya utaratibu wa kuwarejesha madereva waliofungwa nchini Zambia ili waje kutumikia vifungo vyao hapa nchini.Hivi karibuni, chama hicho kilitishia kufanya mgomo kushinikiza kuachiwa huru kwa madereva hao lakini kimesitisha baada ya kubaini kuwa walitoa tamko hilo kinyume cha sheria.


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Clement Masanja alisema madereva 12 walifungwa mwaka jana nchini Zambia baada ya kupatikana na hatia ya kufanya uchakachuaji wa mafuta ya mawese.
Alisema mafuta hayo yalikuwa yanasafirishwa na kampuni ya Dando na kwamba magari 14 yalikamatwa na madereva wawili walifanikiwa kutoroka.  
“Tunaomba serikali itusaidie kufanya utaratibu kati yetu na serikali ya Zambia ili wenzetu waje watumike vifungo vyao hapa nchini,” alisema Masanja.


Alisema pia matajiri wengi wamekuwa wakiwaonea madereva hali iliyosababisha waishi maisha magumu na kuingia kwenye vishawishi kutokana na kipato kidogo.
“Hebu fikiri dereva anasafirisha mzigo kwenda Congo anakaa siku 60 analipwa Sh200,000 tu je ataweza kukidhi mahitaji yake?” alihoji Masanja.
Kuhusu kusitisha mgomo wao, Mwenyekiti huyo alisema walibaini kuwa mtu waliyekuwa wanamshinikiza awaachie huru wanachama wao (kampuni ya Dando) hana uwezo huo kwasababu madereva hao tayari wamo mikononi mwa sheria.


Naye mmoja wa wajumbe wa chama hicho, Hussein Msangi alisema hivi karibuni alienda nchini Zambia na kukutana na baadhi ya wafungwa hao na kwamba wengi wao walikutwa wana hali mbaya kiafya.
“Kuna mwenzetu mmoja anaitwa Edward Mwakibinga tulikuta anaharisha damu na kama ikitokea hata mmoja akafa kuna hatari ya watu kugoma,” alisema Msangi.
Alisema madereva hao wamefungwa kwa shoti ndogo kati ya lita 100 na 160 wakati madereva wengine walikutwa na lita 70 za maji ambazo alidai kuwa ni kitu cha kawaida kwenye mafuta.



HOTUBA YA RAIS KIKWETE

ASIE KUBALI MSHAHARA WA SERIKALI AFUNGE VIRAGO



WAKATI Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka akiendelea na matibabu Afrika Kusini, Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali haihusiki na kilichomtokea daktari huyo kwa kuwa alikuwa kiungo muhimu katika majadiliano baina ya pande hizo mbili.


Rais Kikwete alisema hayo jana katika hotuba yake ya kila mwezi, ambapo mbali na suala hilo, pia alizungumzia sababu za mgomo wa madaktari na usafirishaji wa wahamiaji haramu.


Dk Ulimboka ambaye alikuwa anaratibu mgomo wa madaktari unaoendelea nchi nzima kutokana na Serikali kushindwa kutimiza madai yao mbalimbali, anatibiwa figo na majereha aliyoyapata katika sehemu mbalimbali za mwili, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana, kisha kupigwa, kung'olewa kucha, meno mawili na kutupwa katika Msitu wa Pande, usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita.
Tangu kutokea kwa unyama huo uliofanywa na watu wasiojulikana, baadhi ya wananchi na wanaharakati wamekuwa wakiilaumu Serikali kuwa inahusika na utekaji huo na wengine wakienda mbali zaidi, kuwa watekaji walikuwa wanamlazimisha kueleza nani yuko nyuma ya mgomo wa madaktari. 
Rais Kikwete, kama awali alivyosema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, walisema wanatambua kuwa, Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka kuhusu kilichomtokea Dk Ulimboka, lakini yeye ameshangazwa na hisia hizo, kwani haoni sababu ya Serikali kufanya hivyo.


"Dk Ulimboka alikuwa kiungo muhimu katika mazungumzo baina ya Serikali na madaktari. Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya.  Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam madaktari wanamwamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali," alisema Rais Kikwete.
Alisema Serikali haina sababu ya kumdhuru Dk Ulimboka kwa sababu suala la mgomo, Mahakama Kuu imekwishatoa amri ya kuusitisha, hivyo anayekaidi amri hiyo atakuwa ananunua ugomvi na mhimili huo wa dola, ambao wenyewe una mamlaka ya kumtia adabu.
"Hivi baada ya kufika hapo Serikali iwe na ugomvi na Dk Steven Ulimboka kwa sababu ipi na jambo lipi hata iamue kumdhuru?" alihoji na kuongeza:
"Kama kuna mtu wa Serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake binafsi na siyo za Serikali au kwa kutumwa na Serikali," alisema Rais Kikwete.


Alisema alichofanyiwa Dk Ulimboka kimemsikitisha na kumhuzunisha kwa kuwa ni kitendo cha kinyama na kinyume kabisa na mila na desturi za Tanzania.
Alisema Watanzania hawajazoea mambo hayo na kwamba ameelekeza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane.  
"Nimesema kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa," alisema.
Alisema anatoa mkono wa pole kwa Dk Ulimboka na kumwombea apone haraka ili aungane na familia yake na Watanzania wenzake katika ujenzi wa taifa. 
Rais Kikwete pia alimpongeza Juma Mgaza ambaye alimsaidia Dk Ulimboka kumtoa katika pori alikotupwa na kumpeleka kituo cha polisi kwa moyo wake wa huruma.


KUHUSU MGOMO
Kuhusu mgomo unaoendelea Rais Kikwete alisema, kiwango cha mshahara cha Sh3.5 milioni wanachokitaka madaktari Serikali haina uwezo wa kukitoa, hivyo daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi serikalini bila ya kulipwa mshahara huo, awe huru kuacha kazi na kwenda kwa mwajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho.
Rais Kikwete alisema, kwa sasa Serikali haiwezi kuwaahidi kuwa inao uwezo wa kuwalipa mshahara wa kuanzia wa Sh3.5 milioni na posho zote zile, kwani ikifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa Sh7.7 milioni kwa mwezi, kitu ambacho haitakiweza. 
"Si vyema kutoa ahadi hewa kwa watu tunaowaheshimu na kuwathamini kama walivyo madaktari. Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha. Nasi tutamtakia kila la heri,"alisema Rais Kikwete.


Rais Kikwete alisema, madaktari hawana sababu ya kugoma ili washinikize kulipwa mshahara huo kwani uwezo haupo.
"Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24. Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe," alisema.
Alisema mamlaka za ajira zimeanza kuchukua hatua hizo kwa wale wanaokwenda kinyume na sheria za kazi na wataendelea kufanya hivyo kwa wote wanaoendelea kugoma.  
Alisema anajua baada ya hatua hizo kuchukuliwa kuna manun’guniko ya kuonewa yatajitokeza, lakini ni bora kufanya hivyo ili ijulikane Serikali haina daktari. 


"Mlitegemea mwajiri afanyeje? Ni bora kufanya hivyo ili ajue hana daktari aweze kufanya utaratibu wa kuziba hilo pengo na huyo anayekuja awe na mahali pa kuishi."
Kutokana na hali hiyo amewasihi madaktari kuacha mgomo na kurejea kazini, kwani Watanzania wanateseka na kupoteza maisha. 


SABABU YA MGOMO
Rais Kikwete alisema kwamba, kuna masuala matatu ambayo yamekuwa na mwafaka kwa kiasi fulani na kutoafikiana kwa baadhi ya mambo kati ya madaktari na Serikali.
Alisema suala la kwanza ni suala la kufanya kazi katika mazingira hatarishi ambalo Serikali imekubali hoja ya kuchukua hatua ya kuwalinda madaktari wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi. 


Pia alisema Serikali imeeleza dhamira ya kurudisha posho ya mazingira hatarishi kwa watumishi wa umma wanaostahili na utekelezaji wake utafanyika baada ya uchambuzi wa kina wa kubainisha mazingira hatarishi ni yapi, viwango stahiki viwe vipi na nani hasa wahusike. 
Rais Kikwete alisema kuwa, madaktari wamekataa suala hilo la kufanya uchambuzi, wanataka kiwango kiwe kama wanavyotaka wao, yaani asilimia 30 ya mshahara na kianze mara moja.


Alisema suala la pili ambalo wamekubaliana nusu nusu ni kuhusu nyumba za kuishi ambalo Serikali imekiri wajibu wake wa kuwapatia nyumba za kuishi.  
Rais Kikwete aliongeza kwamba, kwa maeneo ambayo madaktari wanalipwa posho ya pango, Serikali imesema waajiri wataendelea kufanya hivyo kwa mujibu wa taratibu zilizopo kwa watumishi wa umma wenye stahili ya kupewa nyumba.


Alisema jambo hilo limekataliwa na madaktari na kutaka lazima walipwe asilimia 30 ya mshahara kama posho ya nyumba. 
Rais Kikwete alisisitiza kwamba, Serikali kwa upande wake imeona vigumu kufanya hivyo na kuwasihi wakubali wanayotendewa kama wafanyakazi wengine wote wa umma.


Alisema suala lingine ambalo lilikuwa na makubaliano ya nusu nusu ni kuhusu posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu na pande zote mbili ziliafikiana kuwa yapo baadhi ya maeneo nchini yanayo mazingira magumu kwa watumishi wa umma, hivyo hatua zichukuliwe kuwasaidia watumishi hao. 
Kuhusu posho, alisema Serikali imekubali kuwapo posho ya aina hiyo ila itatekelezwa baada ya kufanya uchambuzi wa kuainisha mazingira husika, kutambua watumishi waliopo na gharama zake.
Alisema madaktari hawajakubali kusubiri zoezi la uchambuzi lifanyike, wanataka Serikali ilipe posho hiyo sasa.  


"Tofauti hapa si posho hiyo kuwapo, bali ni rai ya Serikali ya kubaini maeneo yenyewe na kupanga aina ya hatua na viwango vya posho kulingana na mazingira halisi ya maeneo. Madaktari hawaoni haja ya kufanya hayo," alisema.
Alisema kuna mambo mawili ambayo hayakuwa na mwafaka kabisa kati ya pande hizo mbili na la kwanza ni posho ya kuitwa kazini (on call allowance). 
Rais Kikwete alisema, Serikali ilishaongeza posho hizo tangu Februari, 2012 posho iliongezwa kutoka Sh10,000 hadi Sh25,000 kwa daktari bingwa, Sh20,000 kwa dakari mwenye usajili wa kudumu na Sh15,000 kwa madaktari waliohitimu ambao wapo katika kipindi cha mafunzo kazini (Interns). 
Alisema hata hivyo, madaktari kwa upande wao hawakukubali uamuzi huo wa Serikali na kusisitiza walipwe asilimia 10 ya mshahara. 


Rais Kikwete alisema ugumu wa kukubali pendekezo la madakari ni kuwa sharti la malipo haya ni mtu kuitwa kazini na kwamba ukitaka ilipwe kiwango cha mshahara ina maana kuwa hata kama daktari hakupangwa kuitwa au alipangwa na hakutokea aendelee kulipwa.
 Alisema jambo la pili ambalo mwafaka haukufikiwa baina ya Serikali na madaktari ni kuhusu mshahara wa kuanzia kazi wa daktari ambao madaktari wanataka uwe Sh3.5 milioni wakati Serikali inasema kiasi hicho hatukiwezi.
Alisema Serikali imeeleza utayari wake wa kuongeza mshahara kwa kati ya asilimia 15 mpaka 20 kama ambavyo itafanya kwa watumishi wote wa umma katika mwaka huu wa fedha.  
Rais Kikwete alisema, kwa kiwango cha sasa cha mshahara wao, daktari ataanzia kati ya Sh1.1 milioni na Sh1.2 milioni kutegemea kiwango kipi hatimaye kitaamuliwa.
"Madaktari wamekataa katakata na wameng’ang’ania Sh3.5 milioni," alisema.


Alisema ni muhimu madaktari wakatambua kuwa wagonjwa wanateseka na wengine kupoteza maisha kwa mgomo usiokuwa halali kisheria ambao pia haustahili kuwapo hata kwa mujibu wa maadili ya udaktari.
Alisema viongozi wa MAT na wenzao wanawaingiza madaktari katika mgogoro na mahakama na waajiri wao isivyostahili.  
Rais Kikwete alisema ni vyema viongozi wa madaktari na madaktari wakatambua kuwa wanashiriki katika mgomo usiokuwa halali ambao pia kiongozi wao mkuu amekana mahakamani kuwa hahusiki nao. 


Rais Kikwete alisema madaktari lazima watambue pia kwamba ajira zao wanaziweka hatarini kwani mfanyakazi hana kinga ya kutofukuzwa kazi na mwajiri kwa kushiriki mgomo unaokubalika kisheria. 
"Huu siyo. Watapoteza ajira, hawana pa kukimbilia, hawana cha kuwalinda. Kwa madaktari interns, wanahatarisha maisha yao, kwani hawatapata cheti cha kudumu wakishiriki mgomo usiokuwa halali. Lazima watafakari kwa hayo wafanyayo," alisema. 


Saturday, June 23, 2012

DOWNLOAD 2012/13 BUDGET

CLICK HERE TO DOWNLOAD














ALIPUA UFISADI NA MGODI ULIVYOUZWA

SAKATA la ufisadi katika uuzwaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya limeibuka upya, safari hii ikielezwa na Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kuwa umeuzwa kwa bei ya kutupa.Mbunge huyo ambaye ni mwanasheria, amelitaka Bunge kuunda Kamati Teule kwenda kuchunguza ufisadi huo, huku akihoji sababu za Serikali kuutengea mabilioni ya shilingi wakati umekwishauzwa.

Mkono alisema kuwa, “Mgodi huo wenye thamani ya matrilioni ya shilingi, umeuzwa kwa bei ya kutupa ya dola 700,000 tu za Marekani (Sh1.1 bilioni), kwa kampuni ya Intra Energy ya Australia.”

Mgodi wa Kiwira uliwahi kuzua malalamiko baada ya kumilikishwa kwa Kampuni ya ANBEN Limited, mali ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na mkewe, Anna Mkapa, lakini Januari mwaka huu, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja aliieleza Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), kuwa ANBEN Limited haihusiki tena na mgodi huo.

Alifafanua kuwa kampuni hiyo iliondolewa kuwa miongoni mwa wamiliki wa hisa kwa vile haikuweza kulipia hisa 200,000 ilizokuwa imechukua wakati wa usajili wa Kampuni ya Tan-Power Resources (TPR).

Akichangia mjadala wa Bajeti jana, Mkono alihoji sababu za Serikali kutenga Sh40 bilioni kwa ajili ya kulipa watu wa mgodi wa Kiwira ilhali inajua kuwa mgodi huo uliuzwa kwa bei ya kutupwa tangu mwaka 2007.

“Tumetenga Sh40 bilioni za kuwalipa watu waliotuibia fedha zetu, eti tunasema kwamba tunalipa madeni, haya ni madeni gani ambayo tunakwenda kulipa huko?” alihoji Mkono.

Alisema mwaka 2007 wabunge walipiga kelele wakiitaka Kampuni ya Tan Power iliyokuwa mbia wa Serikali katika mgodi huo, kuurudisha serikalini, lakini mwaka jana kampuni hiyo iliuza mgodi huo kwa bei ya kutupa.

“Unauzaje mgodi huu wenye thamani ya matrilioni ya pesa kwa bei hii ya kutupa?” alihoji na kuendelea, "Haya ni mambo ya ajabu sana. Tungeweza kupata fedha nyingi sana kutokana na mgodi huu na fedha hizi zingetusadia katika kugharimia mahitaji yetu ya bajeti.”

Mbunge huyo aliungana na wabunge wengine kuiponda Bajeti ya Serikali kwa kutegemea fedha za wahisani, huku rasilimali za nchi zikiendelea kufujwa bila huruma.

Alisema nakisi inayoonekana kwenye Bajeti, inatokana na uwezo mdogo wa kukusanya fedha za ndani licha ya kwamba nchi ina utajiri mkubwa wa madini, ambayo hata hivyo, yanawanufaisha watu wengine na kuwaacha Watanzania wakitaabika.

Mkono pia aliishambulia Serikali kwamba ‘ilichakachua’ mradi wa uchimbaji wa madini katika mgodi wa Buhemba na kuwadanganya wananchi ambao hawakunufaika na kitu chochote.

Kutokana na hilo, mbunge huyo alisema kuwa Bajeti ya mwaka 2012/13 imetoa upendeleo kwa baadhi ya maeneo huku ikiyaacha mengine muhimu, ambayo yanagusa masilahi ya wananchi.

“Serikali ilichakachua Buhemba lakini inapeleka tena Sh1 bilioni huko na sijui zinakwenda kufanya nini wakati ingeweza kupeleka katika moja ya shule za jimboni kwangu, au hata kama ingetusaidia wananchi wa Mara kujenga chuo kikuu cha kilimo ambacho kinajengwa mkoani kwetu,’’alisema Mkono.

Alisema yeye binafsi haelewi Serikali inaposema haina fedha kwani migodi ya Kiwira na Buhemba ingetumika vizuri, ingeweza kuipatia Serikali kiasi kikubwa cha fedha kinacholingana na fedha zinazotolewa na wafadhili. 

Friday, June 22, 2012


MGOMO WA MADAKTARI KUANZA LEO

JUMUIYA ya Madaktari imetangaza rasmi kuanza kwa mgomo usio na kikomo kuanzia leo, huku ikidai Serikali imekataa kutekeleza madai yao yote yaliyowasilishwa katika kamati ya majadiliano iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.Wakati madaktari hao wakitangaza kurejea rasmi katika mgomo huo uliositishwa miezi mitatu iliyopita, Pinda aliliambia Bunge jana wakati akijibu Maswali ya Papo kwa Papo, kuwa mgomo huo ni batili na haukubaliki.


Saa chache baada ya Pinda kutoa onyo hilo lililorushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni na redio kutoka Dodoma, madaktari hao wakiwa jijini Dares Salaam walitangaza mgomo huo wenye lengo la kushinikiza Serikali kutekeleza madai yao.


Mgomo huo ulitangazwa kwa waandishi wa habari na Dk Stephen Ulimboka, muda mfupi baada ya kukamilika kwa mkutano wa ndani wa madaktari, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Utamaduni la Watu wa Urusi.


Dk Ulimboka alisema mgomo huo usio na kikomo utawahusu madaktari wa kada zote nchini, na unatarajiwa kuanza kesho, baada ya wiki mbili walizotoa kwa Serikali kumalizika bila ya makubaliano yoyote.

“Madaktari kwa ujumla wao wamekubaliana kuwa watarejea katika mgomo usio na kikomo, hii ni kutokana na kugundua kuwa hakuna dhamira ya dhati ya Serikali, kumaliza mgogoro kati yetu na Serikali, uliodumu kwa muda mrefu sasa,” alisema Dk Ulimboka na kuongeza,

Thursday, June 21, 2012


UOZO WA TBS KUANZA KUISHA

SIKU chache baada ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda kuiagiza Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kumsimamisha kazi Mkurugenzi wake Charles Ekelege, shirika hilo limetangaza kampuni zilizopewa kazi ya kukagua magari yanayotoka nje ya nchi.

Mapema mwezi uliopita Dk Kigoda alitoa agizo hilo la kumsimamisha kazi Ekerege ili kupisha taratibu za kisheria ikiwamo uchunguzi kufanyika dhidi yake kutokana na madai ya TBS kuwa na ofisi hewa za ukaguzi wa magari nje ya nchi. 

Sakata la Ekelege liliibuliwa mwanzoni mwa mwaka huu,  ambapo Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC), chini ya Makamu Mwenyekiti wake, Deo Filikunjombe ilimtuhumu mkurugenzi huyo baada ya  kubaini kuwepo kwa udanganyifu kwenye mpango wa TBS wa kukagua bidhaa nje ya nchi.  Filikunjombe alieleza kuwa waligundua madudu baada ya kutembelea vituo vya ukaguzi wa magari nchini Singapore na mjini Hong Kong, China ambapo walikuta vituo hewa vya ukaguzi wa magari.

Lakini jana, shirika hilo  lilitoa tangazo lililotolewa na Kaimu Mkurugenzi wake mkuu, linataja kampuni zilizopewa na zilizopokonywa kazi ya kukagua magari.

Tangazo hilo limeeleza kuwa tangu Juni 18 mwaka huu TBS imefuta leseni Na 0656 ya ukaguzi wa magari iliyokuwa ikifanywa na gereji ya  Jaffar Mohammed Ali iliyopo Dubai ambayo ilikuwa ikikagua magari yanayoingizwa nchini kutoka nchi hiyo.

“Kutokana na tangazo hili wote wanaoingiza magari kutoka Dubai wanashauriwa kupeleka magari yao kukaguliwa na kampuni ya Jabal Kilimanjaro Auto Elect Mechanical, magari ambayo yataingizwa nchini bila kukaguliwa na kampuni hii hayataruhusiwa kuingizwa katika soko la Tanzania,” lilieleza tangazo hilo.

Pia, lilieleza kuwa limefuta leseni Na 0655 ya kampuni ya WTM Utility Services ya nchini Uingereza kujihusisha na ukaguzi wa magari na badala yake magari yote kutoka nchini humo yanatakiwa kukaguliwa na kampuni ya Vehicle Operator Services Agency (VOSA).

“Magari yatakayoingizwa nchini kutokea Uingereza bila kukaguliwa na kampuni hii ya VOSA  hayataruhusiwa kuingia katika soko la Tanzania” lilieleza tangazo hilo.



MTEI AMTETEA JOHN MNYIKA

MWASISI wa Chadema, Edwin Mtei amemtetea Mbunge wa Ubungo, John Myika kuwa alikuwa sahihi kusema kwa Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu, kwa kuwa kuna matukio mengi yaliyohitaji uamuzi wake na hakuutoa kwa wakati.

Pia Mtei amelaumu Kanuni za Bunge zilizomwezesha Naibu Spika, Job Ndugai kumtoa nje ya ukumbi wa Bunge mbunge huyo.

  Juzi, Mnyika alitolewa nje ya ukumbi wa Bunge, baada ya kukukataa kufuta kauli yake kuwa ‘Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu’.
Akitetea kauli hiyo, Mtei alirejea baadhi ya matukio aliyodai yanaonyesha udhaifu huo, ukiwamo uamuzi ya Rais Kikwete juu ya hatua za kuwachukulia walioiba fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Mtei alifafanua kwamba,  kitendo cha Rais  Kikwete kuwataka wezi hao warudishe fedha walizoiba badala ya kuwakamata, kinadhihirisha udhaifu mkubwa wa kiongozi huyo.

  “Rais Kikwete ana udhaifu wa kuwachukulia hatua za kisheria watu ambao wanahujumu taifa  kwa ufisadi…udhaifu wa Rais ni kama kutowadhibiti wezi wa fedha zetu kama fedha za EPA. Aliwaambia wezi warudishe fedha, badala ya kuwatia ndani wanabaki wanatamba kwa kuiba fedha zetu,” alisisitiza Mtei aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu.

 Alisema kibaya zaidi ni kwamba, nchi inayumba kutokana na uongozi mbovu kuanzia ngazi ya urais hadi chini, kwa kuwa tunaongozwa na watu wasiojua na kuisimamia Katiba.

Akitoa maoni yake juu ya Bajeti ya Serikali ya mwaka huu, Mtei alisema Bajeti hiyo haina jipya kwa kuwa haishughulikii matatizo na kero za wananchi.

Alisema Bajeti hiyo ambayo mjadala wake unahitimishwa kesho, haiwezi kukabilina na mfumuko wa bei unaolikabili taifa.

Kuhusu suala la deni la Taifa linalofikia Sh20.2 trilioni, alisema nchi ipo njia panda, hali ambayo ni hatari kwa kuwa ni mzigo kwa taifa na linazidi kuongezeka kila mwaka.

Mwanasiasa huyo ambaye ni Mwenyekiti wa kwanza wa Chadema, aliponda vitendo vya Serikali kukopa fedha kila mara kwenye mabenki ya kibiashara nchini, na kuomba kwa wahisani.



Wednesday, June 20, 2012


KESI YA JUSTINE BEIBER 

JUSTINE BEIBER yuko kwenye hatua ya kutafuta hatma ya kesi yake ya madai ya mpiga picha kupigwa.
Uchunguzi wa Tukio hilo lililotokea MEI 27 mwaka huu umekamili na ushaidi kukabidhiwa kwa waendesha mashtaka. Maofisa wa kesi hiyo hawakuweza kuwasiliana na kijana mwenye miaka 18, JUSTINE BEIBER ili kuwapa nini kilitokea kwa upande wake yeye kama mshtakiwa.


Hata hivyo mashtaka yanayomkabili hayajamzuia POP STAR huyo kuendelea na shughuli zake maana alionekana mjini NEW YORK akiwa na uso wa furaha akisaini AUTOGRAPH kwa mashabiki wake.OFISI mahakama ya mji wa LOS ANGELES sasa ndio inapita kesi hiyo kwa kina na itaangalia kama JUSTINW BEIBER atahukumiwa kama atakuwa na hatia. Mpiga picha huyo alidai alipigwa na JUSTINE BEIBER alipo kuwa akitoka kwenye ukumbi wa sinema Calabas Commons hulo Los Angeles akiwa na mpenzi wake SELENA GOMES.
JB akiwa mwenye uso wa furaha mbele ya mashabiki wake
FANS wa JUSTINE BEIBER wakionyesha albamu ya msanii huyo
JUSTINE BEIBER akiambatana na mpenzi wake SELENA GOMEZ

JAY-Z AFUNGULIWA MASHTAKA

IMEIBUKA mashtaka kwa rapa Jay-z ambaye anadaiwa kutumia kazi ya mwandishi mmoja wa vitabu ambaye amashahili yake yalitumika kwenye kitabu cha nyota huyo.
Katika kesi hiyo iliyofunguliwa Juni 13, Los Angeles Patrick White anamtuhumu RAPPER maarufu Jay-z mwenye miaka 42 kwa kutumia sehemu ya kazi yake na kuitupia kwenye kitabu hiko kama yake Jay-Z ambacho ni kinyume na sheria huku kitabo hiko kikijizolea umarufu mkubwa.

"Mwaka 2009 komputa yangu ilingiliwa (hackers) na kusababisha kazi yangu kunakiliwa kwa sehemu kubwa kutumika kwenye kitabu 'Decoded' ambavyo walitumia maneno mbalimbali, rangi na misemo iliyo kuwa ni kazi. NIlijaribu kuwasiliana na mwandishi alie andika kitabu kile (Decoded) lakini sikupata majibu"

Jay-z na kitabu chake hicho kilicho jizolea kuwa kitabu bora kwenye mauzo mwaka 2010 ambacho kilikuwa na mkusanyiko mashahili ya nyimbo zake za nyuma pamoja na maana zake na kikafanya fizuri kwa mauzo kwenye MtandaO wa AMAZON.

MELI MPYA YA AZAM

Meli hiyo inavyoonekana kwa Nje Meli hiyo inavyoonekana kwa ndani.Meli hiyo inavyoonekana kwa Ujumla---- .Azam yaamua kufanya kweli na hivi karibuni meli ya kisasa iko mbioni  kuzinduliwa ambayo ikawezesha watu kwenda na magari yao Zanzibar. Meli hiyo inauwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.

KAMPUNI ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa ya kisasa kwaajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja. Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa. 

 Mohamedi alisema shida ya usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli hiyo kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari 200 ambapo abiria atakae jisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar es Salaam ataweza kufanya hivyo.



Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe, Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20.


JINSI MNYIKA ALIVYO TIMULIWA BUNGENI

BUNGE jana lilichafuka tena baada ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kusema kuwa Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu, kauli ambayo ilisababisha Naibu Spika, Job Ndugai kuamuru atolewe bungeni.

Mnyika alitoa kauli hiyo wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/13, ambapo alieleza kuwa analazimika kusema Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu, wabunge ni wazembe na nchi imefika hapa ilipo kutokana na upuuzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

"Mimi nasikitishwa na jambo moja, tumefika hapa kutokana udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa bunge na wabunge na tumefika hapa kutokana na upuuzi wa CCM, nasema hivi nina ushahidi.”

Lukuvi/ Ndugai
Kauli hiyo ya Mnyika ndio ilichafua hali ya hewa  bungeni, ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge na Uratibu, William Lukuvi ndipo alisimama na kuomba mwongozo wa Spika.
“Nataka kumbukusha Mnyika, kutokana na kauli zake, kwa kutumia kanuni ya 64 (d) ambayo inaeleza mbunge yeyote hatatumia jina la Rais kwa dhihaka katika mjadala au kulishawishi bunge kwa jambo lolote,” alisema Lukivi.

Aliendelea kufafanua kuwa, “Lugha kwamba Rais Kikwete ni dhaifu, CCM ni wapuuzi nilikuwa naomba, Mheshimiwa Mnyika, miongoni mwa watu ninaowaheshimu sana, nadhani katika hili, amepotoka naomba afute kauli yake.”
Baada ya kauli hiyo ya Lukuvi, Ndugai alifafanua zaidi kuhusu jambo hilo akisema ni kweli kanuni inajieleza vizuri sio tu katika maneno yake pia amelisema vibaya Bunge hilo na kumtaka afute kauli hiyo.

Mnyika alisimama na kuomba apewe nafasi ya kufafanua kauli yake ya kwanini Kikwete ni Rais dhaifu, lakini Naibu Spika, alimuomba afute kauli yake, kitu ambacho mbunge huyo aligoma kufanya, badala yake akasisitiza bunge limpe nafasi ya kufafanua.
Kutokana na uamuzi wa kumtimua Mnyika bungeni.

Ndugai alisema mbunge anapotoa lugha ya matusi au maudhi na akatakiwa na kiti cha Spika afute kauli yake na bado akagoma, ni mamlaka kwa kiti hicho kumtoa nje ya bunge katika muda uliosalia au hata kumsimamisha asihudhurie vikao vitano vya bunge.
Ndugai aliamuru walinzi wamtoe Mnyika nje mara moja na kumzuia asishiriki shughuli yoyote ya bunge hadi kesho saa 3:00 asubuhi.

“Ndugu wabunge tunaongozwa kwa utaratibu, nikitoa uamuzi wangu kwa Kanuni ya 73 (2), ambayo inaeleza kuwa, mbunge au waziri atakayetoa lugha ya maudhi atatatakiwa na Spika ajirekebishe na akikataa atakaa nje kwa muda wote ulisalia katika kikao cha siku hiyo. Nikiwa Naibu Spika ninayejiamini, uamuzi ambao nauchukua sasa, Askari mliopo hapa naagiza mumtoe nje mheshemiwa Mnyika mara moja,” aliagiza Ndugai.

Kabda ya tukio hilo, Mnyika alichangia bajeti hiyo kwa maneno makali dhidi ya wabunge wa CCM wanavyopigania bajeti ya Serikali isiyotekelezeka, huku akiwafananisha na mtu asiye na akili timamu (chizi), kwamba yeye akiendelea kupambana nao ndio ataonekana chizi zaidi.
 “Mtu ukiwa unamkimbiza chizi wewe ndio utaonekana chizi zaidi, hivyo siungi mkono na waache machizi waendelee na uchizi wao,” alisema.

Kauli hiyo ya Mnyika inaonekana kutaka kujibu mapigo ya kikao cha juzi ambapo mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba wakati akichangia bajeti, alisema kuwa wapinzani ni wanafiki, waongo, wana mapepo na wanapaswa kuombewa na kupimwa akili.

Alisema bajeti hiyo haiendani na Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano, ambao ulisainiwa na Rais  Kikwete na pia haiendani na Ilani ya Uchaguzi ya CCM, hivyo akashangaa kauli za wabunge wa chama tawala kuishambulia Bajeti ya Upinzani kwa maneno ambayo aliyasema anaweza kuyafananisha na uchizi.

“Wanasema mipango, unafikia kusema maneno mengine ni ya uchizi uchizi, hivi kutokana na maeneno yaliyotekelezwa, kama ya upinzani haitekelezeki, lakini tumezungumza pensheni ya wazee katika bajeti iliyopita, kwa bahati mbaya wabunge hawa wa CCM sijui hamuwasikilizi hata viongozi wenu?" alihoji Mnyika.

Alifafanua kuwa ,"Suala la malipo ya pensheni kwa wazee, hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwahi kulizungumza mjini Morogoro katika sherehe za wazee, na aliahidi Serikali itakwenda kutoa pensheni ya wazee.  Sasa hapa unaposema haitekelezeki ndio maana unafikia kusema kuna kauli nyingine kama ni za uchizi uchizi hivi."

Alisema pia katika suala la ongezeko la mishahara hadi kufikia 315,000, wamerudia katika bajeti ya upinzani kwani linawezekana, sitaki kutaja hapa takwimu za wafanyakazi wote wa Serikali na malipo yao.

“Lakini, bunge lililopita tulitoa takwimu hapa jinsi ambavyo inawezekana mshahara kima cha chini ufikie 315,000 na ndio sababu leo tumerudia tena, kwani Serikali haijatekeleza, lakini kuna wapofu wa kumbukumbu ambao hawasomi kumbukumbu za bunge," alisema Mnyika.

Tuesday, June 19, 2012


ENEO LA MANZESE

Mfano halisi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi inayoendelea kujengwa kwenye barabara ya Morogoro, katikati ni sehemu ya kituo cha abiria na mabasi ya kasi, pembeni ni barabara ya magari ya kawaida.



NILILAZIMISHWA KUPIGA PENATI

"Usisikie kwenda kupiga penalti...siku zote sitaki kusikia suala hili, kwani pale ni ufundi tu sasa ukikosea kwa kupiga nje au kumlenga kipa, lawama ndugu yangu" anasema Frank Domayo chipukizi wa JKT Ruvu aliyejiunga na Yanga alipokuwa akiitumikia Taifa Stars Msumbiji.

Domayo alifunga penalti ya saba katika mchezo uliomalizika kwa Stars kufungwa penalti 7-6 na Msumbiji katika mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Afrika zitakazofanyika Afrika Kusini baadaye mwakani. Mechi hiyo ilipigwa Uwanja wa Taifa Zimpeto jijini Maputo.

"Nililazimishwa kwenda kupiga penalti baada ya wachezaji wengine kuogopa...mimi siyo mpigaji mzuri wa penalti kwa hiyo baada ya Boko (John) kupiga penalti ya sita na kupata na Msumbiji nao wakapiga wakapata, kila mtu aliogopa kwenda kupiga.
"Ngassa (Mrisho), Samatta (Mbwana) na Haruna (Moshi) wote walikataa wakanilazimisha mimi kwenda kupiga, nikasema poa tu ngoja nikajaribu lakini huku miguu ikinitetemeka.
"Wakati ninakwenda nikawaza, Watanzania wote wananitazama mimi, hizi ndiyo lawama zenyewe ukikosa. Nilipanga nipige upande wa kulia sikubadili uamuzi,  nashukuru Mungu nilifunga.
"Nikawaangalia Ngassa na Boban...Ngassa akaenda kupiga penalti ya nane akapata jamaa wakapata, sasa ikabakia kwa Samata na Haruna wakawa wanasakiziana kwenda kupiga."Mbwana akamwambia Kaseja piga hiyo, lakini naye akasita basi Samatta akaenda kupiga kwa bahati mbaya alikosa kwa kipa kuipangua.
"Kaka ile ni presha tupu, ukisikia mashabiki wanakuzomea wakati unakwenda kupiga penalti unahitaji umakini na utulivu wa hali ya juu kufanya kile unachotaka," alisema Domayo.
Waliopata penalti kwa Stars ni Amir Maftah, Shabaan Nditi, Shomari Kapombe, John Boko, Frank Domayo, Mrisho Ngassa wakati waliokosa ni Aggrey Morris, Kelvin Yondani na Mbwana Samata.
Lakini kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesifu uwezo wa kujituma ulioonyeshwa na wachezaji wake katika mchezo wao wa juzi dhidi ya Msumbiji na kusema: "Wachezaji wangu walicheza vizuri na kujituma kama nialivyotaka.
"Najivunia wachezaji wangu walifanya kile nilichotaka, lakini bahati haikuwa yao inapofika suala la penalti huwa hakuna mwenyewe kwani hata timu kubwa Ulaya zinatolewa.
"Jambo zuri zaidi ni kwamba tumekuja hapa na kufunga mabao kama tulivyowahidi wa Tanzania, kwamba tunakwenda Msumbiji tutapata bao ndicho tulichofanya tena tumepata mabao saba.
Kim aliwapongeza wenyeji kwa kutumia vizuri nafasi yao ya kuwa nyumbani na kupata ushindi huo.
Naye nahodha wa Stars, Juma Kaseja alisema bahati haikuwa yao, lakini sasa ni wakati wa kujipanga upya.

"Timu ni nzuri, tumecheza mechi nne sare moja na Malawi, tukafungwa na Ivory Coast na tumeshinda Gambia kabla ya kufungwa Msumbiji. Nadhani wote mmeona mabadiliko."

"Watanzania wanatakiwa kuwa na subira ili timu iendelee kujiamini kwa sababu kuna wachezaji wengi ni chipukizi na wengi wanacheza vizuri," alisema Kaseja. Naye beki Kelvin Yondan alisifu jinsi walivyojituma na hata kusawazisha bao japokuwa wametolewa kwa mikwaju ya penalti.


Monday, June 18, 2012

KIM HOI KWA KANYE WEST



IMEONEKANA kwamba STAR Kim Kardashian hatimaye kapata kikamilifu mtu katika maisha yake. Uhusiano na Kanye West umeonekana kuboresheka siku hadi siku na wako tayari kufanya mipango ya baadae kuhusu familia yao.


Habari kwamba Kanye West tayari ana mawazo ya kuzaa na Kim, ana uhakika kuwa Kim yuko tayari pia kukubaliana na swala la ndoa.
hata hivyo, Kim ambaye ameachana na mumewe Kris Humphries na hadi sasa kesi ikiwa bado inaendelea mahakamani lkn hadi sasa ikiwa haijapatiwa ufumbuzi wowote na ikiwezekana wapendanao hao wataibuka mahakamani ili kuweka pingamizi ili kesi iweze kwisha na taraka kukubaliwa.


Hata hivyo Kanye West na Kim wako tayari kwa ndoa, kipingamizi ni kesi hiyo hata hivyo watu wengi wamekuwa na maswali mengi kichwani kutokana na maamuzi ya Kim ya kuacha na wanamume pindi anapoelewa. Pia kwa kipindi chote hiki walichokuwa kwenye mahusiano imeonekana Kim kufurahishwa na Kanye huku Kanye West akiwa na uamuzi wa kuzaa na Kim ili kuweka msisitizo kwenye uhusiano wao.





MADONNA AFANYA KUFURU


Ni muhimu kwa msanii mkubwa kujua atafanya nini kwenye shoo ili kuwavuta karibu mashabiki wake. Ila Madonna ni mjanja na anajua ni jinsi gani atakuteka ila kwa upande mwingine inawezekana akawa amepitiliza.


Sasa yuko Instanbul, ambapo alikuwa kwenye stage aki'perfom katika concert yake ambapo alionesha chuchu ya ziwa lake na ilikuwa kwa makusudi kabisa abayo ilichafua picha zilizokuwa zikichukuliwa kwenye "screen" kubwa iliyokuwa hapo uwanjani. baada ya tukio hilo alionesha "tatoo" kwa kuachia mgongo wake kwa sehemu kubwa huku tatoo ikionekana maandisha "NO FEAR".


Alisikika mmoja wa mashabiki wake akisema "Madonna ni mjanja sana anapokuwa stejini sio muoga, anajua kutukonga na namkubali.
Hata hivyo vitendo kama hivyi vilishawahi kuonekana kwa Star mwingine Lady Gaga mwenye kujaa vituko, Madonna bado yuko kwenye Tour yake kubwa ya kuelekea America hata hivyo. 

 
 
Animated Social Gadget - Blogger And Wordpress Tips